Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Wednesday, September 23, 2020

Rais wa Afrika Kusini azitaka nchi tajiri kusaidi uchumi wa nchi za Afrika

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa, ambaye pia ni mweneyekiti wa Umoja wa Afrika ametoa wito kwa mataifa ya dunia kuyasaidia mataifa ya Afrika kujikwamua kiuchumi, kutokana na janga la Corona.

Kiongozi huyo wa Afrika Kusini ambaye nchi yake imeathirika zaidi kutokana na idadi kubwa ya mamabukiziii ya virusi vya Corona, ameonya kuwa iwapo mataifa ya Afrika hayatasaidiwa ikiwa ni pamoja na kufutiwa madeni, yataendelea kuyumba kiuchumi kwa kipindi kirefu.

Kauli hii inaendana na ile ya rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Felix Tshisekedi, ambaye ameyataka mataifa tajiri kusamehe madeni kwa nchi masikini, ikiwa ni pamoja na Afrika wakati huu nchi nyingi zikikabiliwa na janga hatari la Corona.

Licha ya mataifa tajiri zaidi ya 20 na Shirika la Fedha Duniani, IMF, kusema kuwa yanatathmini cha kufanya kuyasaidia mataifa hayo, rais Thsisekedi katika ujumbe wake kwa viongozi wa dunia kupitia njia ya video, ametaka kufutwa kabisa kwa madeni hayo.
Tangazo
ap
Loading...
taboola dsk
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )

End: