Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Friday, September 4, 2020

Tanzania kuwania nafasi ya Ujumbe wa Mfuko wa Pamoja wa Mazao Duniani

Balozi wa Tanzania nchini Uholanzi, Mhe. Irene Kasyanju amemnadi mgombea wa Tanzania anayewania nafasi ya ujumbe kwenye Kamati ya Ushauri ya Mfuko wa Pamoja wa Mazao Duniani (Common Fund for Commodities – CFC) alipotembelea Ofisi za Mfuko huo zilizoko mjini Amsterdam, Uholanzi tarehe 02 Septemba, 2020.

Balozi Kasyanju alikwenda CFC kufanya mazungumzo na pia kumpongeza rasmi Mkurugenzi Mwendeshaji wa CFC, Mhe. Balozi Sheikh Mohammed Belal kwa kushika nafasi ya kuiongoza CFC kwa kipindi cha miaka minne, kazi aliyoianza rasmi mwezi Aprili 2020 baada ya kuchaguliwa kwa kauli moja kushika wadhifa huo wakati wa Mkutano Mkuu wa 31 wa Baraza la Uongozi la CFC uliofanyika tarehe 04 Desemba 2019. 

Katika mazungumzo yao Balozi Kasyanju alimhakikishia Mwenyeji wake huyo ushirikiano wa Tanzania kwa Taasisi yake na kutoa shukrani za dhati kufuatia mikopo yenye riba nafuu iliyotolewa kwa ajili ya kuboresha miradi mitatu inayoendelea hivi sasa nchini Tanzania.

Balozi Kasyanju aliitumia fursa hiyo sawia kumnadi mgombea wa Tanzania, Dkt. Jacqueline David Mkindi, ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa “Tanzania Horticultural Association (TAHA)” iliyoko mjini Arusha.

 Balozi Kasyanju alimuelezea Dkt. Mkindi kuwa ni kiongozi mahiri na mchapa kazi na akadhihirisha kwamba endapo atachaguliwa kushika nafasi hiyo ataiwakilisha vema Tanzania kwa kuwa mshauri bora na makini kwa CFC na Nchi zote Wanachama wa CFC na hivyo kuleta mwamko mpya kwenye Taasisi hiyo muhimu.

CFC iliundwa mwaka 1989 kwa mujibu wa taratibu za Umoja wa Mataifa kwa lengo la kuboresha na kuleta maendeleo kwa jamii ya wakulima na wazalishaji wa bidhaa katika Nchi Zinazoendelea. 

Hivyo basi, CFC imejikita katika kutoa ufadhili wa mikopo kwa ajili ya miradi ya maendeleo kwa kutumia rasilimali zake zinazotokana na michango ya hiari ya Nchi Wanachama na Wafadhili.

Tanzania ni Mwanachama hai wa CFC na katika Taasisi hii inawakilishwa kwenye Baraza lake la Uongozi na Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, kama Gavana; na Balozi wa Tanzania Nchini Uholanzi ambaye ni Gavana Msaidizi. 

Aidha, Tanzania imewahi kushika nafasi ya Mkurugenzi Mwendeshaji wa CFC na vile vile mjumbe wa Kamati ya Ushauri ya CFC zaidi ya miaka 10 iliyopita. 

Hivyo, ni wakati mwingine muafaka kwa Tanzania kushika nafasi kwenye CFC hasa baada ya kutambua kwamba Mkurugenzi Mwendeshaji huyu mpya ameingia na nguvu mpya za kuleta mageuzi kwenye Taasisi yake na kuifanya iwe yenye tija zaidi kwa Wanachama wake.
Tangazo
ap
Loading...
taboola dsk
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )

End: