Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Friday, September 11, 2020

Upatikanaji wa Maji Simiyu Waongezeka Maradufu

juu
Samirah Yusuph
Simiyu.Upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama Mkoani Simiyu  unatarajiwa kuongezeka kutoka  asilimia  51 ya mwaka 2019  hadi  57.4 ifikapo 0ctoba 2020 kupitia mradi wa lipa kulingana na matokeo (PF4R ) hali itakayosaidia wananchi kuepukana na  adha ya upatikanaji wa huduma hiyo kwa uhakika na urahisi.

Ongezeko hilo limesemwa jana  na meneja wa wakala wa maji na usafi wa mazingira vijijini (RUWASA) mhandisi Mariam Majala wakati wa makabidhiano ya mabomba yatakayotumika kutekeleza miradi ya mji Mkoani humo yaliyofanyika katika ofisi za RUWASA mjini Bariadi.

Mhandisi Majala alisema  mpaka sasa wamepokea  asilimia 70 ya mabomba ya maji yenye thamani ya milioni 823 ambayo yatatumika kutekeleza miradi 23 kwa Mkoa mzima huku wakisubiria wakati wowote kuwasili kwa asilimia 40 ya mabomba hayo yaliyobaki.

"hali ya upatikanaji wa huduma ya maji kwa sasa sio mbaya na tunawahakikishia wananchi ongezeko kubwa la huduma ya maji" alisema Majala

Aliongeza kuwa mabomba hayo yatasambazwa vijijini katika halmashauri zote tano za mkoa wa Simiyu ambako uchimbaji wa visima umeshakamilika kwa lengo la kuwasogezea huduma ya maji vijijini.

Awali akikagua mabomba hayo katibu tawala mkoa wa Simiyu Mariam Mmbaga amewataka wananchi kushiriki kwenye mradi huo kwa kutunza miundombinu ya maji ili lengo la ongezeko hilo walilokusudia liweze kufikiwa  huku akiipongeza bodi ya manunuzi kwa kazi nzuri iliyofanyika.

‘’Utandazaji wa mabomba utatoa ajira kwa wananchi, tunawaomba washiriki katika ujenzi wa miradi hiyo pia waitunze na wawe walinzi wa kwanza ili lengo la kuongeza usambajizaji wa maji vijijini tunataka tuone ushiriki wao katika miradi hiyo’’ alisema Mmbaga.

Aidha aliipongeza bodi ya zabuni iliyofanya kazi kwa weledi baada ya kuona mahitaji ya maji katika mkoa huo, huku akiitaka wakala hiyo kuitembelea miradi inayosuasua na kuzipatia ufumbuzi baadhi ya changamoto zinazojitokeza katika miradi hiyo kwa kuzifikisha ngazi ya mkoa hadi Wizarani.
Mwisho.
ap
Loading...
taboola dsk
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )