Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Friday, September 11, 2020

Zingatieni Sheria,kanuni Na Taratibu Za Utumishi Wa Umma - Katibu Mkuu Wizara ya Habari


Na Lorietha Laurence-WHUSM, Dodoma.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari ,Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Hassan Abbasi amewataka watumishi wapya kufuata sheria, kanuni na taratibu  za utumisgi wa umma wakati wa kutekeleza majukumu yao ya kila siku ili kuleta matokeo chanya kwa Serikali.

Dkt. Abbasi ameyasema hayo jana Jijini Dodoma alipokuwa akifunga Mafunzo ya siku tatu yaliyotolewa kwa watumishi hao wa kada ya Habari ikiwa ni tararibu ambazo hufanya kwa kila mwajiriwa mpya wa serikali.

“Natoa rai kwenu hakikisheni mnayaishi na kuyatenda yale yote mliyofundishwa na Wataalamu ili muweze kutekeleza majukumu na kufikia malengo yaliyowekwa na Serikali” Dkt.Abbasi.

Aliongeza kwa kueleza kuwa Wizara hiyo inasimamia sekta za burudani ambazo huwaleta wananchi kwa pamoja na umoja bila kujali kabila wala dini ambapo ni soft power muhimu  ya nchi hivyo  watumishi hao walisisitizwa kuzingatia utaalamu, weledi na ufanisi wakati wa kutekeleza majukumu yao  ili kuleta manufaa kwa Serikali na wananchi  kwa ujumla.

Aidha Dkt. Abbasi aliwataka watumishi hao kuwa mabalozi wazuri katika kutunza siri za serikali , kufanya kazi kwa ushirikiano, kuwa na mahusiano mazuri na watumishi wengine,  kuweka malengo katika utendaji wao wa kazi ndani na nje ya utumishi wa umma ili kuwezesha kufikia malengo yaliyowekwa na Wizara.

Mafunzo hayo yalihitimishwa  kwa kiapo cha uadilifu kwa watumishi wa umma ambacho waliapa mbele ya mwajiri wao ambaye ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Hassan Abbasi.

Mwisho.

ap
Loading...
taboola dsk
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )

End: