Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Thursday, October 8, 2020

Idara Ya Usimamizi Wa Mali Za Serikali Yaimalisha Udhibiti

juu


 Na. Saidina Msangi na Peter Haule, WFM, Dodoma
Serikali imeahidi kutatua changamoto ya uhaba wa Wasimamizi wa Mali za Serikali kutokana na umuhimu wao katika kuisaidia Serikali kusimamia mali zake ambazo ni nyingi.

Hayo yamebainishwa jijini Dodoma na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Mary Maganga, wakati akifungua Kikao kazi cha Wasimamizi wa Mali za Serikali kutoka Mikoa 21 ya Tanzania Bara, kilicholenga kutathimini kazi za Idara hiyo na maeneo yanayotakiwa kuboreshwa.

Bi. Maganga alisema  suala la upungufu wa watumishi wa Idara hiyo limechukuliwa kwa uzito na Serikali hivyo katika maeneo ambayo yanaupungufu mkubwa wa nguvu kazi wataanza kuona watumishi  wakiongezeka kwa kuwa hatua za dhati zimeanza kuchukuliwa.

Amesema kuwa Miongozo iliyotolewa na Idara ya Usimamizi wa Mali za Serikali ikiwa ni pamoja na Mfumo wa Kutunza Kumbukumbu za Mali za Serikali (GAMIS) itasaidia kurahisisha utendaji kazi na kuongeza ufanisi wenye tija katika kujua na kudhibiti mali za Serikali katika maeneo yote nchini.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Idara ya Usimamizi wa Mali za Serikali Bw. Chotto Sendo alisema kuwa Wasimamizi wa Mali za Serikali katika Mikoa yote wanatakiwa kusimamia na kutoa tathmini nzuri kwa Mali za Serikali zinazofutwa kwa kujiridhisha juu ya uchakavu wake kabla ya kuiarifu Wizara kwa ajili ya maamuzi.

Alisema kuwa Idara yake inajukumu la kubuni Sera, kanuni, taratibu na miongozo ya kusimamia mali za Serikali, kutoa Leseni za Udalali, Kusimamia vifaa vya kutunzia mali (Kasiki) pamoja na ufuatiliaji wa mali chakavu ambazo huondolewa kulingana na Sheria na kanuni zilizopo.

Bw.  Sendo alisema kuwa Idara yake ina umuhimu mkubwa kwa Wakuu wa Mikoa kuwa na uhakika wa mali wanazozimiliki, hivyo kuwasaidia katika maamuzi mbalimbali ya kiuongozi katika eneo lao la utawala.

Aliwapongeza watumishi walioshiriki kikao kazi hicho kwa kuwa kina lengo la kupashana habari lakini pia kufahamiana, kupeana miongozo mbalimbali ya majukumu na kujua wajibu wao katika utekelezaji wa majukumu yao.

Kikao kazi hicho cha siku mbili kimewashirikisha watumishi 88 kutoka mikoa 21 ya Tanzania bara wakiwemo Wahakiki Mali na Mafundi Kamonga.

Mwisho.

ap
Loading...
taboola dsk
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )