Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Wednesday, October 21, 2020

Mawakala Wanne CHADEMA Wafariki Ajalini

juu

Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Rukwa, Shadrack Malila, amesema, mawakala wanne wa chama hicho wamefariki dunia katika ajali ya gari iliyotokea barabara ya Molo - Sumbawanga mkoani Rukwa walipokuwa wanakwenda kuapishwa huku wengine watatu wakijeruhiwa.
 
Kamanda wa Polisi mkoa wa Rukwa Justine Masejo, amethibitisha na kueleza kuwa watu watatu wamefariki hapohapo na mmoja amefariki akiwa hospitali.

Aidha ACP  Masejo amesema kuwa majeruhi wanaendelea na matibabu akiwemo dereva ambaye yupo chini ya ulinzi.

Ameongeza kuwa gari iliyopata ajali ni Noah yenye namba za usajili T 381 DZQ, huku chanzo kikiwa ni ugeni wa dereva kwenye barabara hiyo na aliendesha gari kwa kasi hivyo ikamshinda kwenye kona na kupelekea ajali.
chn
ap
Loading...
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )