Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Thursday, October 15, 2020

Mgombea Urais wa CCM, Dkt. Magufuli aahidi kulinda Tunu za Taifa


Mgombea urais kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Dkt. John Magufuli ameahidi kulinda tunu za Taifa zilizoachwa na Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ikiwa ni kuenzi tangu alipofariki miaka 21 iliyopita.

Dkt. Magufuli amesema hayo jana wakati wa kampeni katika Uwanja vya Tanganyika Packers akiomba ridhaa ya wana-CCM na wananchi kumchagua kuwa Rais kwa awamu ya pili na kuchagua wabunge na madiwani wa CCM kwa miaka mitano ijayo.

Tunu hizo ni Pamoja na uhuru wa Taifa la Tanzania, amani na utulivu, umoja na mshikamano, Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, ujenzi wa Taifa la kujitegemea lenyewe kwa kutumia rasilimali zake.

“Kwa kutumia hiyo misingi mitano serikali ya awamu ya tano katika miaka mitano iliyopita imejitahidi kuyatekeleza maono ya Baba wa Taifa. Nitakapochaguliwa kuongoza Tanzania nitahakikisha tunu hizi nazilinda kwa nguvu zetu na hasa muungano wetu.”

Katika hatua nyingine mgombea huyo wa urais amesema wananchi wa Jimbo la Kawe wakimchagua mgombea ubunge wa jimbo hilo, Askofu Josephat Gwajima, serikali yake itatenga fedha kwa ajili ya kijenga bandari ya katika Jimbo hilo.

chn
ap
Loading...
taboola dsk
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )