Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Thursday, October 1, 2020

Msajili Avionya Vyama vya siasa vinavyotaka kuungana siku ya Oktoba 3 mwaka huu


Msajili Msaidizi wa Vyama vya Siasa nchini Sisty Nyahoza, ameviasa vyama vya siasa vinavyotaka kuungana siku ya Oktoba 3 mwaka huu, kuacha mara moja mpango huo kwani wanakiuka utaratibu wa sheria na kwamba walianza vizuri hivyo ni vyema kila mmoja akaendelea kunadi sera zake.

Nyahoza ametoa kauli hiyo hii leo Oktoba Mosi, 2020, kwenye kipindi cha Supa Breakfast ya East Africa Radio na kuongeza kuwa hata hivyo tayari Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa imekwishaviandikia barua vyama hivyo kwa kuwa ni masuala ya kiofisi huwa hawaziweki barua hizo hadharani.

"Kwanza tunaawaasa hao wanaotaka kufanya hivyo tarehe 3 sisi kama walezi wa vyama vya siasa kwa sababu wanakiuka sheria, walianza vizuri hivyo kila mmoja aendelee kunadi sera yake na wagombea wao wa urais", alisema Nyahoza.

Amesema sheria ya vyama vya siasa inawekwa kwa maslahi ya wanachama na wananchi na unapotaka kushirikiana hutakiwi kufanya kitendo chochote kinachohadaa wananchi kwa hiyo ni kosa kufanya hivyo ghafla wakati wa uchaguzi.

“Ukiunganisha nguvu na chama kingine wakati mmeshakubaliana na wananchi kwamba mtatekeleza sera gani ni kuwahadaa, sisi tulishawasiliana nao na tukawaambia waache," alisema Msajili Msaidizi wa Vyama vya Siasa nchini Nyahoza.

Vyama vya siasa vya upinzani vya ACT-Wazalendo na Chama Cha Demokrasia na Mandeleo (Chadema) vimekuwa vikitajwa kuwa na mpango wa kumuunga mkono mgombea mmoja wa urais Oktoba 3, licha ya kuwa vyama vyote hivyo vimeshasimamisha wagombea wao wa urais.

chn
ap
Loading...
taboola dsk
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )