Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Wednesday, October 28, 2020

Polisi Wamkamata na Kumwachia Halima Mdee

Jeshi la Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni asubuhi ya leo Jumatano tarehe 28 Oktoba 2020 walimkamata Mgombea Ubunge wa Kawe, Halima Mdee wa Chadema kufuatia sintofahamu iliyojitokeza katika zoezi la upigaji kura jimboni humo.

 Taarifa zinaeleza, Mdee alikamatwa katika Kituo cha Kawe kufuatia sintofahamu hiyo kutokea baada ya mgombea huyo kudai kuona masanduku ya kura yakiwa na kura zilizopigwa kinyume na utaratibu.

Akizungumzia sakata hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Edward Bukombe amesema, mgombea huyo alihojiwa baada ya kukamatwa kisha akaachiwa huru.

Kuhusu madai ya Mdee ya sanduku kukutwa na kura feki, Kamanda Bukombe amesema hawajapokea taarifa hizo.

.

chn
ap
Loading...
taboola dsk
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )