Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Sunday, October 11, 2020

Simu Janja Zitumike Kutafutia Fursa - Dkt Chaula

juu

 Na Faraja Mpina – WUUM, Dar es Salaam
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Mawasiliano) Dkt. Zainab Chaula ameiasa jamii ya kitanzania kutumia simu janja kutafutia fursa mbalimbali za kujitafutia kipato ili kuinua uchumi binafsi na  nchi kwa ujumla.

Dkt. Chaula alizungumza hayo alipokuwa akifunga Kongamano la Nne la Mwaka la TEHAMA lililofanyika jijini Dar es Salaam Oktoba 7 hadi Oktoba 9, 2020.

“Tuzitumie simu janja vizuri kwa kutafuta fursa za kutuinua kiuchumi, tusitumie  simu hizo kuperuzi kwa ajili ya burudani pekee bali tufunguke, tutafute fursa za kiuchumi kwa kutumia simu janja zilizounganishwa na mtandao ili maendeleo yapatikane kwa mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla”, alizungumza Dkt Chaula

Dkt Chaula ametoa rai kwa  wadau kutoka taasisi za umma na binafsi walioshiriki katika Kongamano hilo kutekeleza yale yaliyo ndani ya uwezo wao, wasiiachie Serikali ifanye kila kitu kwasababu fursa nyingi zinapatikana kwa wadau hao ,na kuwaasa wasitoe fursa kwa kufahamiana bali kwa kila mtanzania anayekidhi vigezo kulingana na Katiba, sheria na taratibu za nchi.

Aidha, Dkt. Chaula aliliambia Kongamano hilo kuwa, Wizara imepokea maoni yote yaliyotolewa na kuahidi kuyafanyia kazi kwa haraka, uaminifu na uadilifu mkubwa, ili fursa zilizobainishwa na masuala mengine yaliyojadiliwa ambayo yanahitaji  mkakati wa kidijitali, kwa kushirikiana na wadau mkakati huo utaandaliwa na kutekelezwa kwa wakati.

Naye Mhadhiri kutoka Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT), Dkt. Moses Mwasaga amesema kuwa  matumizi stahiki ya simu janja yatawezesha watu wengi zaidi kuingia na kushiriki kwenye uchumi wa kidijitali kwa kupata huduma mbalimbali na kutengeneza ajira kama ilivyo kupitia mfumo wa miamala ya fedha kupitia simu ya mkononi, ambapo watu wengi wameweza kujiajiri kama mawakala wa kutoa huduma hiyo muhimu, ambayo hapo awali ilikuwa ikitolewa na benki pekee.

ap
Loading...
taboola dsk
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )