Samirah Yusuph
Simiyu.Mamlaka ya kuzuia na kupambana na rushwa mkoani Simiyu imefanikiwa kurejesha kiasi cha shilingi milion 22 kati ya milioni 30 ambazo zilitolewa na ubalozi wa Marekani kwa ajili ya kusaidia Vikundi vya wanawake wajane na wenye maambukizi ya UKIMWI.
Fedha hizo zilitolewa na ubalozi wa Marekani kwa vikundi vya wanawake ili kuwawezesha kujiinua kiuchumi kwa kuwawezesha kununua mashine za kufyatua tofali wilayani Maswa mkoani hapo.
Baada ya andiko la mradi lililoandikwa na Raphael Chichalo mwalimu wa shule ya Nyalikungu, ambaye ni mme wa mwenyekiti wa kikundi hicho ambacho kilikusudiwa kupata pesa Kwa kivuli cha taasisi isiyo ya kiserikali ya WODEG.
Hata hivyo baada ya kupata pesa hizo hazikupelekwa katika miradi iliyo kusudiwa badala yake zilitumika kama pesa ya familia.
Ambapo katika taarifa ya robo ya kwanza ya mwaka kiserikali 2020/2021 Mkuu wa Takukuru mkoa wa simiyu Joshua Msuya alisema wamefanikiwa kurejesha fedha hizo katika awamu mbili ili ziwafikie walengwa.
"Pesa hizo zimerudishwa kwa awamu mbili mara ya kwanza walirudisha milioni 15 awamu ya pili milioni saba na bado milioni nane ambazo na hizo pia watazirejesha," alisema Msuya.
Katika hatua nyingine amewatahadharisha wananchi kuelekea uchaguzi mkuu kujiepusha na vitendo vya rushwa pamoja na kutun a kadi zao za kupigia kura kwa kuepuka kuvunja kanuni na sheria za uchaguzi.
Mwisho.

Loading...
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi
==>>... << BOFYA HAPA Kui Install>>
Mgid
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )