Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Wednesday, October 14, 2020

Tangazo la Nafasi za Masomo Shule ya sekondari Bigabiro inayomilikiwa na Kanisa la FPCT

juu

Shule ya sekondari Bigabiro inayomilikiwa na Kanisa FPCT tunayo furaha kuwatangazia Washirika,waumini wa Kanisa na Jamii kwa Ujumla nafasi za Masomo.Nafasi zilizopo ni kama ifuatavyo;

1.Kujiunga au Kuhamia kidato cha kwanza na cha tatu 2020 ( Nafasi bado Zipo)

2.Kuhamia kidato cha Kwanza,cha Pili, Cha Tatu au Cha Nne 2021 ( Karibu sana)

3.Nafasi kwa Wanaorudia Mitihani (Reseaters na QT).

Shule yetu ni miongoni mwa shule zinazofanya vizuri mkoani Kigoma,kwani mitihani ya taifa mwaka 2019 wanafunzi walifaulu wote ( Yani asilimia 100 ya wanafunzi wote). Shule inawalimu mahili wanaofundisha masomo ya sanaa,sayansi,lugha na elimu ya biblia.

Kwa kuzingatia uchumi wa wazazi, shule imepunguza ada hadi kufikia 350,000/= kwa mwaka ambayo hulipwa kwa awamu nne.

Shule yetu ni ya kutwa, lakini kuna nafasi ya kuishi shuleni kwa kuzingatia utaratibu utakaopewa na ofisi.

Pia, tunawatangazia wazazi wote wenye watoto waliohitimu darasa la saba kuwa, mwezi October tutakuwa na mafunzo ya awali (Pre-Form One) ambayo yataanza tarehe 15/10/2020.Gharama za Pre form one ni 15,000/=

Mtoto akifika, atapewa T-shirt,Daftari,Kalamu na Penseli.Nafasi zipo kwa watakaotaka kukaa shuleni kwa utaratibu wataopewa shuleni.

Mlete mwanao apate malezi bora ya kitaaluma na kiroho..

Kwa mawasiliano, Piga;

0756 696788- Mkuu wa Shule.

0783 397279- Makamu Mkuu wa Shule.

0265 971183-Mtaaluma


 


ap
Loading...
taboola dsk
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )