Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Waziri Mkuu mstaafu Awamu ya Nne, Mizengo Pinda, amewataka watafiti nchini kuwezesha wakulima kutambua mazao lishe yanayoweza kulimwa katika maeneo yao ili kupambana na utapiamlo na afya duni kwa wananchi.
Waziri Mkuu Mstaafu Pinda amesema hayo jana Oktoba 12,2020 Katika mdahalo uliokutanisha wadau mbalimbali ikiwemo UNICEF, UN, FAO, Taasisi binfasi kuelekea siku ya chakula duniani oktoba 16 mwaka huu uliofanyika chuo kikuu cha Dodoma.
Amebainisha kuwa watafiti wana sehemu kubwa ya kufanya kupitia taaluma yao badala ya kuishia katika maandishi na badala yake waunge mkono wakulima kwani kilimo ni uti wa mgongo.
Kuhusu mikoa iliyoathirika Zaidi na utapia mlo na lishe duni amesema takribani mikoa 15 huku Mbeya, Njombe Rukwa ikitajwa kuwa na hali mbaya Zaidi ambapo amesisitiza ushirikishwaji wa makundi mbalimbali kama vyombo vya habari, Wizara ya Afya na wakulima wenyewe kukabili changamoto hizo.
Naye Mwakilishi Msaidizi wa Shirika la Chakula Duniani,FAO,Tanzania upande wa miradi,Charles Tulahi AMESEMA BAADHI YA NCHI BARANI AFRIKA ZINA UHABA WA CHAKULA
Afisa Lishe kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP ) Neema Shosho amesema Shirika limeanzisha miradi katika mkoa wa Dodoma na Singida kuhakikisha kunakuwa na chakula cha kutosha kuanzia ngazi ya Kaya hadi Taifa.
Kwa upande wake Mwakilishi wa Shirika la kuhudumia watoto Duniani[UNICEF]Bi.Ruth Nkurlu amesema tatizo kubwa la udumavu lina uhusiano na uzazi mama anapojifungua anakuwa na upungufu wa damu ,malezi mama anapozaa anaelemewa na mzigo mkubwa wa kulea na tatizo jingine ni uzazi katika umri mdogo .
Pia Bi.Ruth ametaja changamoto tatu zitokanazo na masuala ya lishe kuwa ni pamoja na udumavu,uzito,na upungufu wa damu kwa akina mama huku akibainisha mpango UNICEF ni kuboresha huduma ya chakula katika kuhakikisha kila Mtoto anapata cha kula kwa wakati sahihi.
Mhadhiri wa chuo kikuu cha kilimo ,Sokoine University of Agriculture ( SUA) kilichopo mkoani Morogoro Theresa jumbe, amesema bado kunachangamoto ya elimu juu ya masuala ya Lishe Katika jamii.
Maadhimisho ya siku ya chakula Duniani yanatarajia kufanyika kitaifa Mkoani Njombe huku kauli mbiu ya mwaka 2020 ikiwa ni Kesho njema inajengwa na lishe bora endelevu.