Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Monday, November 9, 2020

Rais Dk.Hussein Ali Mwinyi Akimuapisha Makamo Wa Pili Wa Rais Wa Zanzibar Leo.


 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Hussein Ali Mwinyi amemwapisha Hemed Suleiman Abdullah kuwa Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar.
Dk Mwinyi amemuapisha kiongozi huyo leo November 9,2020 Ikulu mjini Unguja.

Hafla hiyo imefanyika baada jana November 8, Dk Mwinyi kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya kifungu Namba 39 (1) na 39 (2) cha Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984  Abdullah kuwa Makamu wa Pili wa Rais.

Kabla ya Uteuzi huo,  Abdulla alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba.

Katika hafla hiyo viongozi mbalimbali walihudhuria, akiwamo Katibu Mkuu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Dk Abdulhamid Yahya Mzee, Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Dk Mwinyi Talib Haji na  Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Hassan Khatib.

Wengine ni Naibu Kadhi Mkuu Sheikh Hassan Othman Ngwali, Meya wa jiji  la Zanzibar Saleh Juma Kinana, Viongozi wa vikosi vya SMZ  pamoja na  viongozi mbalimbali kutoka Idara na taasisi  za Serikali.


 

chn
ap
Loading...
taboola dsk
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )