Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Friday, November 13, 2020

Rais Dr Magufuli Aahidi Kumpa Ushirikiano Mkubwa Rais wa Zanzibar Dr Hussein Mwinyi


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli ameahidi kufanya kazi kwa ukaribu mkubwa na Rais wa Zanzibar na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dr. Hussein Mwinyi.


Rais Magufuli ametoa ahadi hiyo leo Novemba 13, 2020, wakati akihutubia na kufungua bunge la 12, kwenye ukumbi wa Bunge jijini Dodoma.

“Nitashirikiana na Rais wa Zanzibar Dkt. Hussein Mwinyi kulinda amani, hatutakuwa na utani hata kidogo na mtu atakayetaka kuvuruga amani na kuingilia uhuru wetu, na namuahidi Rais Dkt. Mwinyi nitampa ushirikiano wa kutosha katika kukamilisha aliyoyaahidi”, amesema.

Aidha Rais Magufuli amesisitiza kuwa serikali yake itaendelea kuboresha mazingira kwa wananchi kuongeza kipato chao ikiwemo mazingira wezeshi ya biashara.

''Katika miaka mitano hii serikali ninayoiongoza itafungua milango ya majadiliano na sekta binafsi na wafanyabishara wote ili kujadili namna ya kuondoa migogoro ya biashara ili tutengeneza mabilionea wengi wakiwemo wabunge'', ameongeza.

Tangazo
ap
Loading...
taboola dsk
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )

End: