Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Friday, November 13, 2020

Rais Magufuli Aitakia Kila la Heri Timu ya Taifa Stars Dhidi ya Tunisia Pamoja na Bondia Mwakinyo


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr John Magufuli amesema  kuwa katika kipindi cha miaka mitano ijayo Serikali itatenga kiasi kidogo cha fedha katika kuziandaa timu mbalimbali za Taifa na pia alitumia fursa hiyo kwa kuitakia heri Taifa Stars kwenye mchezo wake wa leo dhidi ya Tunisia.

 
Dr Magufuli ameyasema hayo leo tarehe 13 Novemba, 2020, wakati wa hotuba ya ufunguzi wa Bunge la 12 jijini Dodoma ambayo ilitoa dira ya uongozi wake katika kipindi cha miaka mitano ijayo.

“Tutaanza kutenga fedha kidogo kidogo kwa ajili ya kuzianda timu zetu za Taifa na katika hilo napenda kutumia fursa hii, kuitakia heri timu yetu ya Taifa kwenye mechi yao dhidi ya Tunisia hapo baadaye,” alisema Magufuli.

Aidha Rais Magufuli aliongezea kwa kumtakia heri bondia Mtanzania Hassan Mwakinyo ambaye anashuka ulingoni hapo baadaye, kupambana na bondia kutoka nchini Argentina kwenye pambano la raundi 12 la ubingwa wa mabara wa IBF.

“Na pia nataka kumtakia heri mwanamasumbwi wetu, Hassan Mwakinyo anayepambana leo, watanzania tunataka ushindi tumechoka kushindwa,” aliongezea Magufuli.

chn
ap
Loading...
taboola dsk
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )