Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Friday, November 13, 2020

Rais Magufuli: Nchi Yetu Iko Salama


Rais  Magufuli amesema katika awamu yake ya kwanza madarakani alihakikisha nchi inakuwa na  amani huku akivipongeza vyombo vya ulinzi na usalama kwa kulinda mipaka ya nchi.

Ameeleza hayo leo Ijumaa Novemba 13, 2020 bungeni mjini Dodoma katika hotuba yake ya kulizindua Bunge.

Amesema Watanzania wameendelea kuwa wamoja licha ya kutofautiana katika dini, kabila na itikadi ya vyama vya siasa.

“Wakati naingia madarakani kulikuwa na wimbi kubwa la mauaji ya kutumia silaha mfano matukio ya Kibiti lakini kutokana na kazi kubwa iliyofanywa na vyombo vya dola yalikomeshwa na kwa sasa nchi yetu ipo salama.


“Nchi yetu imeendelea kuwa kisiwa cha amani na mipaka yake imebaki kuwa salama. Navipongeza vyombo vya ulinzi na usalama kwa kazi kubwa waliyofanya ya kusimamia amani na niwashukuru pia Watanzania kwa kutoa ushirikiano kwa vyombo hivi.” Amesema

chn
ap
Loading...
taboola dsk
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )