Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Tuesday, December 29, 2020

Joe Biden: Trump ameharibu idara muhimu za usalama


Vitengo muhimu vya usalama vimefanyiwa uharibifu mkubwa chini ya utawala wa rais Donald Trump , rais mteule wa Marekani Joe Biden amesema.
 

Biden amesema kwamba timu yake haipati habari inazohitaji kutoka kwa idara ya ulinzi wakati ambapo inajiandaa kuchukua madaraka.
 

Kiongozi huyo mteule ametoa kauli hiyo wakati akizungumza baada ya kupatiwa habari na Maafisa wa Usalama pamoja na wale wa masuala ya sera za kigeni.

Biden anatarajiwa kuapishwa Januari 20, mwakani kuwa rais, hata hivyo Rais Trump amekataa kukubali kushindwa katika uchaguzi wa mwezi Novemba.

Kwa wiki kadhaa baada ya uchaguzi huo wa Novemba 3 , Biden alizuiliwa kupata habari muhimu za kijasusi , ikiwa ni muhimu na utaratibu wa kawaida katika mchakato wa kumkabidhi rais mteule madaraka.

Kufuatia matamshi ya Joe Biden siku ya Jumatatu , kaimu waziri wa ulinzi Christopher Miller amesema kwamba maafisa wamekuwa wakifanya kazi kwa utaalamu mkubwa kuunga mkono mpito.

chn
ap
Loading...
taboola dsk
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )