Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Sunday, December 20, 2020

Mabadiliko Ya Manaibu Makamishna Wa Uhifadhi Wawili Wa Mamlaka Ya Hifadhi Ya Ngorongoro


Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Dkt. Damas D. Ndumbaro (Mb), kwa mamlaka aliyonayo kwa mujibu wa Sheria ya Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, Sura Na. 284,  tarehe 19 Disemba, 2020 amefanya mabadiliko ya Manaibu Makamishna wa Uhifadhi wawili wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA), kwa lengo la kuboresha utendaji kazi wa Taasisi hii.

Katika mabadiliko hayo, Mhe Waziri amemteua Dkt. Christopher D. Timbuka, kuwa Kaimu Naibu Kamishna (Uhifadhi, Utalii na Maendeleo ya Jamii). Kabla ya uteuzi huo, Dkt. Timbuka alikuwa Kamishna Mwandamizi wa Uhifadhi wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA), Kanda ya Kusini. Anachukua nafasi ya Bw. Ephraim A. Mwangomo ambaye amerejeshwa TANAPA.

Aidha,  Mhe Waziri amemteua Bw. Audax R. Bahweitima, kuwa Kaimu Naibu Kamishna wa Uhifadhi (Huduma za Shirika). Kabla ya uteuzi huo, Bw. Bahweitima alikuwa Mchumi Mkuu katika Idara ya Sera na Mipango, Wizara ya Maliasili na Utalii. Anachukua nafasi ya Bw. Abdallah O. Kiwango ambaye amerejeshwa TANAPA.

Uteuzi huo unaanza rasmi  tarehe 19 Disemba, 2020.

chn
ap
Loading...
taboola dsk
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )