Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Monday, December 14, 2020

Mahakama ya Mafisadi Yaahirisha Hukumu ya Ayub Kiboko na Mkewe


Mahakama Kuu Divisheni ya Uhujumu Uchumi na Rushwa maarufu kama Mahakama ya Mafisadi, imeahirisha kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili mfanyabiashara Ayubu Kiboko na Mkewe Pilly Mohamed hadi Desemba 18 mwaka huu.

Uamuzi wa kuahirisha kesi hiyo umetolewa na Msajili wa mahakama hiyo David Ngunyale baada ya washtakiwa hao kufikishwa mahakamani hapo kwa ajili ya kusikiliza hukumu ya kesi yao  iliyotarajiwa kutolewa leo baada ya upande wa mashtaka kufunga jalada la ushahidi lililokuwa na mashahidi 16.

Katika Kesi ya msingi namba 29/2018, Kiboko na mkewe wanadaiwa kukamatwa Mei 23 mwaka 2018 eneo la Tegeta Nyuki – Masaiti wilaya ya Kinondoni jijini Dar es salaam wakiwa wanasafirisha dawa za kuÄşevya aina ya heroin zenye uzito wa gramu 251.25 kinyume na sheria
.

chn
ap
Loading...
taboola dsk
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )