Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Friday, December 25, 2020

Waliomuua kiongozi Chadema wahukumiwa kunyongwa hadi kufa

Mahakama ya Hakimu Mkazi Geita, imewahukumu kunyongwa hadi kufa, washtakiwa 4, akiwemo Alphan Kyalubota, Epafla Mapinda, Mashimu Omary na Kululinda Richard, kwa kosa la kumuuwa kwa kukusudia aliyekuwa Mwenyekiti wa CHADEMA, mkoani humo Alphonce Mawazo, aliyeuawa mwaka 2015.


Hukumu hiyo imetolewa  Desemba 24, 2020, na Hakimu Mkazi Mwandamizi mwenye mamlaka ya ziada Frank Mahimbari, baada ya kujiridhisha kutokana na ushahidi uliotolewa mahakamani hapo kutoka kwa mashahidi upande wa Jamhuri.

Katika shauri hilo namba 9 la mwaka 2019, mshatakiwa wa nne, Habibu Feruzi, ameachiwa huru baada ya ushahidi uliotolewa mahakamani hapo kushindwa kuthibitisha kuhusika kwake kwenye mauaji hayo ya kukusudia hivyo kutokuwa na kesi ya kujibu.

Baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa waliojitokeza kufuatilia kesi hiyo, wamesema kuwa wameridhishwa na hukumu hiyo huku wakiipongeza serikali kwa kutenda haki kwa watu wote bila kuangalia itikadi ya chama.


chn
ap
Loading...
taboola dsk
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )