Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Wednesday, December 16, 2020

Wasajili Wasaidizi Wa NGOs Waaswa Kuzingatia Maadili


 Na Mwandishi wetu Dodoma.
Wasajili wasaidizi wa Mashirikia Yasiyo ya Kiserikali (NGOs) wametakiwa kuzingatia weledi na misingi ya Uzalendo katika utendaji kazi wao huku wakitanguliza maslahi ya Taifa.

Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu, Jijini Dodoma wakati akifungua mafunzo kwa Wasajili wasaidizi kutoka mikoa ya Dodoma, Singida, Tabora pamoja na Wizara zinazosimamia mashirika hayo.

Dkt. Jingu amesema wasajili wa NGOs lazima wazingatie weledi na kufuata taratibu, sheria, kanuni na miongozo katika utendaji kazi wao.

Amesema Sekta ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali ni muhimu kwa maendeleo ya nchi hivyo wasajili wana jukumu la kuhakikisha wanasimamia vizuri kwa kuweka mazingira wezeshi kwa mashirika kutekeleza shughuli zao nchini  na kutanguliza maslahi ya Taifa.

“NGO ni Sekta muhimu katika kila sekta, zinatoa mchango mkubwa katika maendeleo ya nchi yetu, ndiyo maana tupo hapa ni jukumu letu kama Maafisa wa Serikali na waratibu katika maeneo yetu kujipanga kusimamia  kwa weledi,  kuzingatia maslahi ya Taifa, Kanuni na Sheria zilizopo” amesema Dkt. Jingu.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Dkt. Laurean Ndumbaro amewataka washiriki kukumbuka kuwa wasajili wasaidizi ni watumishi wa Umma, wanawajibika kwa Serikali na Wananchi hivyo, wahakikishe wanafuata misingi na taratibu za Utumishi wa Umma.

Ameongeza kuwa watumishi wa Umma wanatakiwa kuzingatia maadili kwa kufuata Kanuni na Sheria mbalimbali zilizowekwa ikiwemo Sheria ya NGOs.

"Ni wajibu na lazima kujituma na   kufanya kazi kwa juhudi na maarifa ili tuweze kutimiza majukumu yetu" Alisema

Mmoja wa Wasajili wasaidizi waliohudhuria mafunzo hayo Dominic Joseph amesema walitarajia kujifunza vitu vingi kwani wamekuwa wakipitia changamoto mbalimbali wakiwa wanaratibu NGOs
maeneo yao na kuwashukuru Makatibu Wakuu wa Afya na Utumishi ambao wamewapitisha kwenye Kanuni na Sheria za kuzingatia kusaidia Watanzania.

“Wametusaidia kutupa shule ya namna ya kutambua umuhimu wa utumishi wetu katika kuhakikisha tunasimamia maslahi ya Taifa na kutanguliza uzalendo tukiwa tunaratibu NGOs, tunashukuru sana kwani wengi hatukuwahi kupata mafunzo kama haya”.

Wizara ya Afya - Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii imeendelea kutoa mafunzo kwa Wasajili Wasaidizi wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali katika ngazi za Mikoa na Halmashauri kwa lengo la kuwawezesha kutekeleza Majukumu yao kutokana na Sheria namba 3 ya mwaka 2019 pamoja na mwongozo wa uratibu wa NGOs wa mwaka 2020.

MWISHO

chn
ap
Loading...
taboola dsk
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )