Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Tuesday, January 26, 2021

Mbunge Kiswaga Aahidi Maendeleo Jimbo La Kalenga Mbele Ya Waziri Mkuu


Na Fredy mgunda,Iringa.
Mbunge wa jimbo la Kalenga mkoani Iringa ameahidi kufanya kazi za kimaendeleo na kuleta maendeleo ya kwa wananchi wa jimbo hilo mbele ya waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa.

Akizungumza mbele ya wananchi wa kijiji cha  Ifunda wakati wa ziara ya waziri mkuu,Mbunge wa jimbo Kalenga Jackson Kiswaga alisema kuwa ameomba nafasi ya kuwa mbunge kwa lengo la kuhakikisha anashirikiana na wananchi kuleta maendeleo kwenye jimbo hilo.

Kiswaga alisema kuwa anamikakati imara na mizuri ambayo itasaidia kukuza uchumi kwa wananchi kwa kuhakikisha anatatua changamoto mbalimbali zilizopo kwenye jimbo hilo.

 Aliongeza kuwa ili kukuza uchumi wa wananchi wa jimbo hilo yampasa ajitahidi kuhakikisha anatatua Mara kwa Mara changamoto ambazo zinarudisha nyuma maendeleo ya wananchi.

Aliwambia waziri mkuu kuwa ubunge wake atautumia kuhakikisha anatatua changamoto za wananchi wa jimbo lake na kutoa mchango mkubwa kwa nchi kwa ujumla kulingana na wajibu aliopewa.

"Mimi kiswaga kama kiswaga nimekuja jimbo la Kalenga kuswaga maendeleo kama jina langu lilivyo hivyo hapa hakuna kula ni kuhakikisha naswaga maendeleo kwa kwenda mbele"alisema kiswaga

Kwa upande wake waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa alisema kuwa mbunge kiswaga ameaminiwa kuwawakilisha wananchi bungeni hivyo anapaswa kufanya kazi na kutatua changamoto za wananchi wa jimbo la Kalenga.

Mheshimu waziri mkuu alisema kuwa anaimani na mbunge huyo kufanya kazi viziri za kuhakikisha anatatua changamoto za wananchi na kuwatengenezea njia ya kufanya kazi za kimaendeleo.

Alisema kuwa anauhakika kuwa kiswaga ataleta mabadiliko katika jimbo hilo kutokana na jina lake na uchapaji kazi alionao kabla hata hajawa mbunge wa jimbo hilo.Tangazo
ap
Loading...
taboola dsk
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )

End: