Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Saturday, January 16, 2021

Museveni Atangazwa Mshindi wa Urais Uganda


 Yoweri Kaguta Museveni ametangazwa kuwa mshindi katika uchaguzi wa rais uliofanyika nchini Uganda Alhamisi wiki hii, akipata asilimia 58.6 ya kura zote. 

Mshindani wake wa karibu, Robert Kyagulanyi maarufu kama Bobi Wine amekuja katika nafasi ya pili akiwa na asilimia 34.8. 

Bobi Wine amesema uchaguzi huo ulikumbwa na ghasia na udanganyifu. Wagombea wengine wa urais hawajafikisha hata asilimia tano. 

Museveni aliyeingia madarakani mwaka 1986 baada ya kundi la waasi alilloliongoza kuyashinda majeshi ya serikali, akimaliza muhula huu atakuwa ameiongoza Uganda kwa miaka 40, na kuwa miongoni mwa marais waliodumu mamlakani kwa muda mrefu zaidi barani Afrika. 

Wakati Tume ya Taifa ya Uchaguzi ikiyatangaza matokeo hayo mchana Jumamosi, makaazi ya Bobi Wine yaliyoko nje kidogo ya mji mkuu, Kampala yalikuwa yamezingirwa na wanajeshi.

Tangazo
ap
Loading...
taboola dsk
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )

End: