Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Wednesday, January 27, 2021

Taarifa Kwa Umma kuhusu Kikao Cha Waziri Wa Kilimo Na Maafisa Kilimo Wa Mikoa Na Halmashauri


Wizara ya Kilimo imeandaa kikao kazi cha Waziri wa Kilimo na Maafisa Kilimo wa Mikoa na Halmashauri nchini kwa lengo la kujadili changamoto za upatikanaji huduma za ugani na nini kifanyike kuwasaidia wakulima kuboresha kilimo ili kiwe na tija.


Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Waziri wa Kilimo Mhe. Prof. Adolf Mkenda (Mb) imesema kikao hicho kitajadili na kuweka mikakati ya utekelezaji wa kuhakikisha wizara inaleta mapinduzi makubwa na kukifanya kilimo kuwa cha kisasa na chenye faida kwa mkulima kwa kuzingatia Programu ya Kuendeleza Sekta ya Kilimo Awamu ya Pili (ASDP II).


Mkutano huo utafanyika tarehe 29-30 Januari ,2021 katika ukumbi wa Mikutano wa LAPF Jijini Dodoma kuanzia saa 3.00 asubuhi.Katika kikao hicho Wizara itaelezea vipaumbele na mwelekeo wake katika kipindi cha miaka mitano ijayo  (2020-2025).


Imetolewa na;
Gerald M. Kusaya
KATIBU MKUU

Tangazo
ap
Loading...
taboola dsk
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )

End: