Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Sunday, February 14, 2021

Baraza la Seneti Lashindwa Kumtia Hatiani Donald Trump


Baraza la seneti nchini Marekani limemuondolea mashataka rais wa zamani wa nchi hiyo Donald Trump, ya kuchochea shambulio baya dhidi ya jengo la bunge, kufuatia vurugu zilizosababishwa na kushindwa kwake katika uchaguzi.

Maseneta 57 walipiga kura ya kumtia hatiani rais huyo wa zamani huku 43 wakikataa mashtaka dhidi yake. Warepublican saba waliunagana na Wademocrat wote kumtia hatiani Trump, lakini idadi hiyo ilikuwa chini sana ya kihunzi cha theluthi mbili iliyohitajika.

Matokeo hayo yameacha migawiko isiyo na utatuzi nchini humo kuhusiana na siasa za Trump zilizosababisha shambulio baya zaidi la ndani dhidi ya mmoja ya mihimili mitatu ya demokrasia ya Marekani.

Ingawa aliondolewa hatia kuhusu shitaka pekee la kuchochea uasi, kesi hii ilishuhudia idadi kubwa zaidi ya maseneta kuwahi kupiga kura kumtia hatiani rais wa chama chao kwa makosa makubwa na madogo

Tangazo
ap
Loading...
taboola dsk
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )

End: