Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kesho Jumapili Machi 28, 2021 atapokea taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) za mwaka wa fedha 2019/20.
Pia, atapokea taarifa ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) ya mwaka 2019/20.
Taarifa iliyotolewa na mkurugenzi wa mawasiliano ya Rais Ikulu, Gerson Msigwa inaeleza kuwa tukio hilo litarushwa moja kwa moja na vyombo vya habari vya redio, televisheni na mitandao kuanzia saa 4:00 asubuhi.
Hafla ya kupokea taarifa hiyo itafanyika Ikulu Chamwino mkoani Dodoma.
Loading...
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi
==>>... << BOFYA HAPA Kui Install>>
Mgid
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )