Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Tuesday, April 6, 2021

Waliochoma chanjo ya corona tu ndio wataruhusiwa kuhiji Mecca mwaka huu


Mamlaka za nchini Saudi Arabia zimesema watu waliopata chanjo ya corona peke yake ndio wataruhusiwa kufanya ibada ya Hija mwaka huu huko Mecca.

Wizara ya Hija na Umrah imetoa taarifa kuwa watu waliopata chanjo pekee ndio watakuwa na vigezo vya kujihi mwaka huu katika mji mtakatifu wa Mecca.

"Watu ambao tayari wamepata chanjo dozi mbili za COVID-19, na wale ambao wamepata chanjo dozi moja ya corona siku 14 kabla ya Hija au mtu ambaye ametoka kupona corona", wizara imesema.

Wizara hiyo imesema pia kuwa itazingatia taratibu zote za kujikinga dhidi ya maambukizi ya corona.

Haijawekwa wazi kama sera hiyo itaendelea mpaka wakati wa Hija kuu baadae mwaka huu.

Saudi Arabia imeripoti kuwa na maambukizi ya virusi vya corona zaidi ya watu 393,000 na zaidi ya vifo 6,700 vinavyotokana na virusi hivyo.

Wizara ya afya ya taifa hilo imesema watu zaidi ya milioni tano wamepata chanjo dhidi ya corona, katika taifa lenye watu zaidi ya milioni 34.

Credit:BBC

Tangazo
ap
Loading...
taboola dsk
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )

End: