Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Friday, May 28, 2021

Mawaziri Biashara, Viwanda, Fedha Na Uwekezaji Kukutana leo Jijini Arusha

Na Mwandishi wetu, Arusha
Baraza la Mawaziri la kisekta la Biashara, Viwanda, Fedha na Uwekezaji (SCTIFI) kutoka nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kujadili wanategemea kukutana leo tarehe 28 Mei 2021 Jijini Arusha kujadili masuala mbalimbali ya kukuza biashara na uwekezaji ndani ya Jumuiya hiyo.

Mkutano huo wa Mawaziri umetanguliwa na mkutano wa Makatibu Wakuu wa sekta ya Biashara, Viwanda, Fedha na Uwekezaji (SCTIFI) wa Jumuiya hiyo uliofanyika jana jijini Arusha ambapo pamoja na mambo mengine, viongozi hao wamepokea na kujadili ripoti mbalimbali ikiwemo ripoti za baraza la kisekta la mawaziri wa fedha, ripoti ya kamati ya forodha, ripoti ya kamati ya biashara, ripoti ya kamati ya viwango ya Afrika Mashariki, ripoti juu ya masuala ya ushindani pamoja na ripoti ya kamati ya uwekezaji.

Mkutano wa Makatibu Wakuu wa jana tarehe 27 Mei 2021 utafuatiwa na Mkutano wa Baraza la Mawaziri wa kisekta tarehe 28 Mei 2021 jijini Arusha
.

Tangazo
ap
Loading...
taboola dsk
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )

End: