Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Thursday, May 20, 2021

Pakistan, Iran Zaahidi Kuimarisha Diplomasia Ya Uchumi


Na Mwandishi wetu
Pakistan na Iran zimeahidi kuendelea kuimarisha diplomasia ya uchumi na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa maslahi mapana ya pande zote.

Ahadi hizo zimetolewa kwa nyakati tofauti wakati Mabalozi wa Pakistan na Iran walipokutana kwa mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula (Mb) katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam.

Mabalozi waliokutana na Waziri Mulamula ni Balozi wa Pakistani hapa nchini Mhe. Mohammad Saleem pamoja na Kaimu Balozi wa Irani hapa nchini Mhe. Hossein Alvandi Behineh ambapo viongozi hao wamejadili masuala ya kuimarisha uhusiano baina ya Tanzania na Nchi zao lakini pia kuimarisha na kuboresha diplomasia ya uchumi kwa maslahi mapana ya nchi zote.

Pamoja na mambo mengine, Balozi wa Pakistan Mhe. Saleem ameelezea kufurahishwa na uhusiano mzuri uliopo baina ya Iran na Tanzania na amepongeza hatua mbalimbali ambazo Serikali ya Tanzania imeendelea kuzichukua katika kuimarisha diplomasia ya uchumi.

Nae Kaimu Balozi wa Iran amesisitiza juu ya uwekezaji na biashara ambapo amesema kuwa Serikali yake ipo tayari kufanya biashara na Tanzania na kuinua uchumi wa wananchi wan chi zote mbili.

Kwa upande wake Balozi Liberata Mulamula (Mb) amewahakikishia mazingira salama ya biashara na uwekezaji na kuwaahidi ushirikiano wa kutosha kutoka Tanzania.

Kadhalika, Waziri Mulamula amesema ushirikiano wa diplomasia ya uchumi kati ya Tanzania na Pakistan unatoa fursa nyingi ikiwemo kukuza biashara hasa katika sekta ya kilimo ikiwemo chai, pamba, korosho, mbegu za mafuta, Madini ya Tanzanite, pamoja na uwekezaji.

chn
ap
Loading...
taboola dsk
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )