Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Monday, May 10, 2021

Wajumbe wa Kamati ya Mradi wa Kuhimili Mabadiliko ya Tabianchi watakiwa kupitia changamoto

 


Wajumbe wa Kamati ya Kitaalamu ya Mradi wa Kuhimili Mabadiliko ya Tabianchi kwa kutumia Mifumo Ikolojia Vijijini (EBARR) wametakiwa kupitia changamoto zote za utekelezaji wa mradi huo zilizojitokeza na kupendekeza hatua za kuchukua.

Wito huo umetolea leo Mei 10, 2021 na Mkurugenzi wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais, Dkt. Andrew Komba alipokuwa akifungua Kikao cha Kamati ya Kitaalamu ya mradi huo jijini Dodoma.

Dkt. Komba alisema kazi kubwa ya kikao hicho kupitia taarifa za utekelezaji wa mradi wa EBARR, matumizi ya fedha, mpango kazi na bajeti ya mradi kwa mwaka 2021 pamoja na kutoa mapendekezo kwa kamati ya uendeshaji wa mradi (Project Steering Committee - PSC) kwa ajili ya maamuzi.

Alisema Tanzania ni miongoni mwa nchi zinazoathiriwa na mabadiliko ya tabianchi ambayo yameonekana katika sekta mbalimbali za uzalishaji nchini ikiwemo kilimo, mifugo, maji, nishati, maliasili, miundombinu na usafirishaji.

Alizitaja athari hizo kuwa ni ukame, mafuriko, maporomoko ya udongo, ongezeko la joto, kuibuka na mlipuko wa magonjwa ya mazao, mifugo na binadamu na uwepo wa viumbe vamizi na kuwa jamii maskini hasa za vijijini huathiriwa zaidi na mabadiliko ya tabianchi.

“Katika kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi, serikali kupitia ofisi ya makamu wa rais inaratibu utekelezaji wa mradi wa ebarr kwa kushirikiana na sekta nyingine za kilimo, mifogo, na maji na halmashauri za wilaya nne tanzania bara na wilaya moja zanzibar.

“Mradi unatekelezwa katika wilaya za Mvomero (Morogoro), Simanjiro (Manyara), Kishapu (Shinyanga), Mpwapwa (Dodoma) na Kaskazini A, (Unguja). Maeneo ya mradi yalichaguliwa kwa kuzingatia maeneo yanye ukame yenye jamii za wakulima, wafugaji, na wavuvi,” alisema.

Aidha, Mkurugenzi huyo alibainisha kuwa chini ya mradi wa - EBARR, Kamati ya Uendeshaji wa Mradi (PSC) hukutana kila mwaka kujadili na kupitisha maamuzi mbalimbali.

kabla ya PSC, Kamati ya Kitaalamu (Project Technical Committee -PTC) hukutana kupitia, kujadili na kutoa mapendekezo kwa ajili ya maamuzi ya PSC kuhusu utekelezaji wa mradi.Tangazo
ap
Loading...
taboola dsk
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )

End: