Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Tuesday, June 1, 2021

Waziri Nchemba: Upekuzi Wa Wateule Ni Endelevu


Na, Saidina Msangi, WFM, Dodoma.
Serikali imesema kuwa siyo sahihi kuwa na Kanzidata ya Upekuzi (Benki ya Waliopekuliwa) ili kurahisisha mchakato wa upekuzi kwa kuwa utendaji na mienendo ya maafisa hubadilika kuendana na wakati husika.

Hayo yameelezwa bungeni jijini Dodoma na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), alipokuwa akijibu swali la Mheshimiwa Jerry William Silaa, Mbunge wa Ukonga alieitaka Serikali kuanzisha Benki ya waliopekuliwa kwa ajili ya uteuzi ili kurahisisha zoezi la uteuzi wa Bodi za Taasisi na kuziwezesha Taasisi hizo kwenda na kasi ya Mhe. Rais kwa kile alichosema kuwa upekuzi umekuwa kisingizio cha kuchelewesha uteuzi.

“Upekuzi kwa ajili ya kujaza nafasi mbalimbali hufanyika kwa wakati husika kutokana na ukweli kwamba utendaji na mienendo ya maafisa pia hubadilika kutoka wakati mmoja hadi mwingine,” alifafanua Mhe. Nchemba.

Aidha, alieleza kuwa Wizara ya Fedha na Mipango ina jumla ya Taasisi 28 ambazo inazisimamia, kati ya hizo, Taasisi Tisa (9) Bodi zake zimemaliza muda wake.

Mhe. Nchemba alisema kuwa mapendekezo ya majina kwa ajili ya kujaza nafasi za Wenyeviti na Wajumbe wa Bodi hizo yamewasilishwa kwenye Mamlaka za Upekuzi.

Mwisho.

Tangazo
ap
Loading...
taboola dsk
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )

End: