Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Friday, July 16, 2021

Majaliwa: Tutaendeleza Mahusiano Na Shirikisho La Mpira Wa Miguu La Morocco


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema Tanzania kupitia Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) litaendelea kuimarisha mahusiano na Shirikisho la Mpira wa Miguu la Morocco ili kukuza kiwango cha mpira huo nchini .

Amesema hayo jana (Alhamisi Julai 15, 2021) baada ya kutembelea Ofisi za Shirikisho hilo na eneo la Mchezo wa Mpira wa Miguu la Mohammed wa VI kuona uwekezaji wa miundombinu ya mpira wa miguu uliofanywa katika eneo hilo.

Sponsored: Top Tanzania Government Jobs You Can’t Afford To Miss!!….Apply now before they expire! 

 

Amesema kuwa Shirikisho la Mpira wa Miguu la Morocco liendelee kutumia fursa ya mafunzo kwa pande zote mbili lengo likiwa ni kuwa na timu za taifa zilizo bora na zenye ushindani kama ilivyo kwa timu ya taifa ya Morocco.

Aliongeza kuwa shirikisho hilo limekuwa likiisadia sana Tanzania katika kujifunza mbinu mbalimbali za kiutawala pamoja na mbinu za kimichezo kupitia timu za taifa za Tanzania.

“Timu zetu za taifa za Taifa Stars, Serengeti Boys, Ngorongoro na Twiga Stars zimekuwa zikija hapa Morocco kuweka kambi kwa gharama ya Serikali yao,  hili ni jambo kubwa na la kuendeleza”

Kadhalika Waziri Mkuu alisema kuwa katika mazungumzo yake na Waziri Mkuu wa Morocco Saad Dine El Otmani alikumbushia ahadi ya Mfalme wa nchi hiyo juu ya ujenzi wa uwanja wa mpira wa miguu wa Mohammed VI uliopangwa kujengwa jijini Dodoma “tumemkumbusha na ameahidi kulifanyia kazi ikiwa ni pamoja na kumkumbusha mfalme ili ujenzi uanze kwa kuwa kila kitu kipo tayari”


Tangazo
ap
Loading...
taboola dsk
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )

End: