Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Thursday, July 1, 2021

Mfugale kuzikwa Julai 5 mkoani Iringa


Mwili wa aliyekuwa  Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), Mhandisi Patrick Mfugale utazikwa  Julai 5, 2021 nyumbani kwake Ifunda mkoani Iringa.

Mfugale alifariki dunia Jumanne Juni 29, 2021 saa 5 asubuhi katika Hospitali ya Benjamin Mkapa jijini Dodoma.

Kwa mujibu wa ratiba ya mazishi, mwili wa Mfugale unatarajiwa kusafirishwa kwenda jijini Dar es Salaam Alhamisi Julai Mosi, 2021 ukitokea Dodoma na kupelekwa katika Hospitali ya Jeshi Lugalo.

Ijumaa Julai 2, 2021 mwili utatolewa hospitalini hapo na kupelekwa viwanja vya Karimjee ambapo wafanyakazi wa Tanroads na Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi watatoa heshima zao za mwisho kisha utapelekwa Kimara Temboni nyumbani kwake.

Baada ya misa takatifu siku ya Jumamosi Julai 3, 2021 mwili wa Mfugale utasafirishwa kwenda Ifunda mkoani Iringa ambapo unatarajiwa kuwasili Julai 4 na maziko yatafanyika Julai 5, 2021 nyumbani kwake Ifunda.

Tangazo
ap
Loading...
taboola dsk
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )

End: