Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Saturday, July 10, 2021

Waziri Simbachawene Aruhusu Kutumika Kwa Nyumba Za Askari


Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi George Simbachawene ameruhusu askari polisi kuanza kutumia nyumba za kisasa zenye uwezo wa kukaliwa na familia zaidi ya 300 zilizopo eneo la Kunduchi na Mikocheni mkoani Dar es salaam.

Waziri Simbachawene amesema hayo wakati wa ziara yake ya kukagua mradi huo wa nyumba za kisasa za makazi ya askari.

Amesema kuanza kutumika kwa nyumba hizo kutasaidia kupunguza uhaba wa nyumba za askari, na kutaleta ufanisi kwa askari wanapotekeleza majukumu yao ya kazi za Kipolisi.

Kwa upande wake mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini Simon Sirro amesema zaidi ya miaka mitatu imepita tangu kukamilika kwa mradi wa ujenzi wa nyumba hizo.

Amesema baadhi ya nyumba hizo kwa sasa zimeanza kuchakaa kutokana na kutokaliwa kwa muda mrefu, pamoja na kukosa matunzo.

Tangazo
ap
Loading...
taboola dsk
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )

End: