Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Thursday, August 26, 2021

Kamati Ya Bunge Yaagiza Mbunge Jerry Silaa Akamatwe


Kamati ya Bunge ya Haki Maadili na Madaraka ya Bunge imeamuru kukamatwa kwa Mbunge wa Ukonga (CCM), Jerry Silaa baada ya kutofika mbele ya kamati hiyo kuhojiwa juu ya shauri lake. 

Silaa alihojiwa mara ya kwanza na kamati hiyo Agosti 24, 2021 ambapo mwenyekiti wa kamati hiyo Mwakasaka alimtaka kurudi tena leo Alhamisi kuendelea na mahojiano.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Alhamisi Agosti 26, 2021 mwenyekiti huyo amesema ameomba kibali cha kukamatwa kwa mbunge huyo baada ya kutofika katika shauli lake.

Mwakasaka amesema Silaa hakutoa taarifa za kutofika kwake na kwamba kamati hiyo ilimsubuiri hadi saa 8.00 mchana,  hivyo wamemwomba Spika kutoa kibali cha kukamatwa kwake na kufikishwa katika kikao cha kamati hiyo kesho saa 4.00 asubuhi.
.

Tangazo
ap
Loading...
taboola dsk
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )

End: