Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Monday, August 30, 2021

Marekani yashambulia gari lenye vilipuzi Kabul,Afghanistan

Marekani imesema imeizuia gari iliyokuwa imebeba shehena ya vilipuzi kwa kuishambulia kutoka angani ikiwa mjini Kabul hapo jana. 

Hayo yameripotiwa saa chache baada ya Rais wa Marekani Joe Biden kuonya kuwa kuna uwezekano wa kutokea shambulio lingine la kigaidi katika mji huo mkuu wa Afghanistan. 

Marekani imedai kuwa imeilenga gari pekee. Lakini vyombo vya habari vya Afghanistan vimeripoti kuwa kuna uwezekano raia pia wamejeruhiwa. 

Siku ya Alhamisi, mshambuliaji wa kujitoa muhanga kutoka kundi linalojiita Dola la Kiislam IS aliwalenga wanajeshi wa Marekani waliokuwa wakizuia umati mkubwa wa watu kuingia uwanja wa ndege wa Kabul, wakijaribu kuikimbia nchi hiyo. 

Tangu Taliban kunyakuwa madaraka, takriban watu 114,000 wameshahamishwa.

-DW

Tangazo
ap
Loading...
taboola dsk
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )

End: