Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imeifuta kesi ya uchochezi iliyokuwa inamkabili, Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleao (Chadema) Tanzania Bara, Tundu Lissu na wenzake wanne.
Ni baada ya Mkurugenzi wa Mashtaka nchini Tanzania (DPP) kuieleza mahakama hiyo kuwa hana nia ya kuendelea na mashtaka dhidi ya washtakiwa hao.
Mbali na Lissu washtakiwa wengine walikuwa ni Mhariri wa Gazeti la
Mawio, Simon Mkina, Jabir Idrisa na Mchapishaji wa Kampuni ya Jamana,
Ismail Mehbooh
Washtakiwa hao kwa pamoja Walikuwa wanakabiliwa na mashtaka matano
likiwamo la kuandika habari za uchochezi kinyume na sheria ya magazeti
ya mwaka 2002.
Loading...
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi
==>>... << BOFYA HAPA Kui Install>>
Mgid
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )