Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Thursday, October 28, 2021

Umoja wa Afrika wasimamisha uanachama wa Sudan baada ya mapinduzi ya kijeshi


Umoja wa Afrika umetangaza  kwamba umesimamisha uanachama wa Sudan katika Umoja huo wa mataifa wanachama 55 baada ya mapinduzi ya kijeshi kuiondoa madarakani serikali ya mpito siku ya Jumatatu. 

Kulingana na taarifa ya baraza la usalama na amani la Umoja huo, hatua hiyo inaanza kutekelezwa mara moja na kuizuia Sudan kufanya shughuli zozote za Umoja wa Afrika hadi kurejeshwa madarakani kwa serikali ya mpito inayoongozwa na raia. 

Baraza hilo la amani na usalama pia limemtaka mwenyekiti wa Umoja huo kumtuma mjumbe nchini Sudan ili kuwasiliana na wadau nchini humo kuhusu hatua zinazohitajika ili kuharakisha kurejesha utaratibu wa kikatiba nchini humo.

Tangazo
ap
Loading...
taboola dsk
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )

End: