Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Tuesday, November 23, 2021

Wafanyabiashara Wa Nyama Wa Oman Kuzuru Tanzania


Wafanyabiashara maarufu nchini Oman wanatarajiwa kufanya ziara nchini tarehe 25 Novemba 2025 kwa ajili ya kukamilisha taratibu za kupata eneo mkoani Tanga la kukusanyia mifugo hai ya kusafirisha Oman kupitia bandari ya Tanga.
 
Wafanyabiashara hao ambao ni Mkurugenzi Mwendeshaji wa Abu Suleiman Al-Darai Trading &Services, Bw. Mohamed S. Aldarai; Afisa Mtendaji Mkuu wa Desert Cold Store LLC, Dkt. Munawar H. Pardhan; Mkurugenzi wa Desert Cold Store LLC, Bw. Aasim M. Pardhan na Mkurugenzi wa IKTIMAl Trading Company LLC, Bw. Salem Al Dighaishi awali walikuwa wanasafirisha nyama iliyogandishwa tani 240 kwa mwezi kutoka nchini walifanya mazungumzo na Balozi wa Tanzania nchini Oman, Mhe. Abdallah Kilima hivi karibuni kuhusu taratibu za utekelezaji wa biashara yao hiyo.
 
Mhe. Balozi aliwapongeza wafanyabiashara hao kwa kuonesha nia ya kufanya biashara na Tanzania kwani itasaidia kubadilisha urari wa biashara kati ya nchi hizi mbili ambao kwa sasa inaonesha Oman inauza zaidi nchini Tanzania. 

Aliwaahidi wafanyabiashara hao kuwa atawakutanisha na Mamlaka husika nchini Tanzania akiwemo Mkurugenzi wa Idara ya Diplomasia ya Uchumi katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Edwin Rutageruka ili kukamilisha taratibu husika.
 
Wafanyabiashara hao walielezea malengo yao ya baadaye ni kufanyabiashara ya kusafirisha matunda kutoka nchini kwenda Oman na nchi nyingine za ghuba, jambo ambalo litasaidia wakulima wa Tanzania kupata soko na kuondoa uharibifu wa matunda yanayoharibika kwa kukosa soko.

Tangazo
ap
Loading...
taboola dsk
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )

End: