Mkoa wa Iringa wenye kumiliki asilimia 40 ya misitu ya kupandwa nchini Tanzania na ni moja ya sehemu zenye aridhi bora sana kwa ajili ya kilimo cha miti duniani. Ili kutumia fursa hii mkoa wa Iringa umeandaa kongamano kubwa la uwekezaji katika sekta ya misitu.
Akifungua kongamano hilo
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alitoa pongezi kubwa kwa mkoa na pia kueleza
msimamo wa Serikali ya awamu ya sita katika kuchochea uwekezaji nchini.
Pia Waziri Mkuu aliagiza makampuni yenye kuchakata mazao ya misitu
kuhakikisha yanatengeneza bidhaa bora na kutosafirisha bidhaa ghafi.
Waziri Mkuu aliuelezea mkoa
wa Iringa kama eneo bora la uwekezaji likiwa na muunganiko mzuri wa
barabara na muda mfupi ujao kwa ndege baada ya kukamilika kwa uwanja wa
ndege wa Iringa.
Mkuu wa Mkoa wa Iringa Queen
Sendega alisema mkoa wake uko tayari kusaidia wafanya biashara kufanya
biashara kwa urahisi kwa kuweka mazingira wezeshi.
Kabla ya kufungua kongamano
hilo alizindua chapa ya Iringa woodland ikiwa ni lengo la mkoa wa Iringa
kuchagiza ukuaji wa utengenezaji wa bidhaa za mbao, kuutangaza mkoa na
pia utalii.
Akizungumza wakati wa
uzinduzi huo Mkurugenzi Mkuu wa Gofin Ventures Imani Kajula ambao ni
waandaaji wa kongamano hilo na mkakati wa kujenga chapa ya Iringa
woodland alisema ” hii ni fursa pana kwa mkoa wa Iringa kufaidika na
sekta ya utalii, misitu na pia kuutangaza mkoa wa Iringa ndani na nje ya
Tanzania” pia kutoa ajira kwa vijana ambao watatumia chapa ya Iringa
woodland kutengeneza bidhaa mbali mbali
Loading...
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi
==>>... << BOFYA HAPA Kui Install>>
Mgid
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )