Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Friday, November 5, 2021

Waziri Wa Nishati Afanya Mazungumzo Na Totalenergies


Waziri wa Nishati, January Makamba amekutana na kufanya mazungumzo watendaji wa kampuni ya TotalEnergies ambayo hujishughulisha uzalishaji na uuzaji wa nishati ulimwenguni.

Watendaji hao wakiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji  wa TotalEnergies Tanzania, Jean Francois Schoepp walifika Wizara ya Nishati kutambulisha rasmi mabadiliko yaliyofanyika ndani ya kampuni hiyo ambapo kwa sasa badala ya kujikita kwenye mafuta na gesi pekee, wameanza kujishughulisha na masuala ya nishati jadidifu pia.

Kampuni hiyo ilimweleza Waziri wa Nishati nia ya kuwekeza Tanzania kwenye miradi ya kuzalisha umeme kwa kutumia nishati jadidifu kama vile Jua na Upepo kutokana na uhakika wa upatikanaji wa vyanzo hivyo vya nishati ya umeme.

Waziri wa Nishati ameieleza kampuni kuwa nia ya Serikali ni kuwa na umeme wa uhakika unaotokana na vyanzo mbalimbali ikiwemo Nishati Jadidifu hivyo kinachotakiwa ni kufanya taratibu zitakazowawezesha kufanya uwekezaji huo.

Tangazo
ap
Loading...
taboola dsk
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )

End: