Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Friday, December 24, 2021

IGP Sirro Awataka Askari Kutenda Haki Na Kutimiza Wajibu Wao

 


Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro amewataka askari Polisi kutimiza wajibu wao kwa kutenda haki kwa wananchi wanaowahudumia na kuvitendea haki vyeo vipya walivyovipata kwa kuhakikisha wanatimiza na kufuata sheria, kanuni na taratibu za nchi.

IGP Sirro amesema hayo leo akiwa katika kambi ya medani ya kambapori iliyopo wilaya ya Siha mkoani Kilimanjaro, wakati akifunga mafunzo ya Kozi ya Uongozi Mdogo Ngazi ya Cheo cha Koplo wa Polisi ambapo jumla ya askari 1697 wamehitimu mafunzo hayo na kutunukiwa Cheo hicho cha KOPLO.

Naye Mkuu wa Shule ya Polisi Moshi SACP Ramadhan Mungi amesema shule hiyo ilipokea jumla ya wanafunzi 1712 na waliofanikiwa kuhitimu mafunzo hayo ni 1697 huku wengine 15 wakiachishwa mafunzo kutokana na sababu mbalimbali.

Aidha amesema mafunzo waliyopatuiwa yatasaidia kuwaongezea weledina maadili  na kupandisha viwango vyao vya uadilifu, uwaminifu, utii haki na uzalendo pamoja na kudumisha ukakamavu, ujasiri na nidhamu katika utendaji wa kazi zao za kila siku.

Tangazo
ap
Loading...
taboola dsk
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )

End: