JESHI
la Polisi Mkoa wa Singida Singida limefanya misako mbalimbali yenye
kulenga kuimarisha ulinzi na usalama ambapo katika misako hiyo limeweza
kuwakamata wahalifu wanaojihusisha na biashara ya madawa ya kulevya na
wizi wa vitu mbalimbali.
Misako hiyo ilifanywa na jeshi hilo kuanzia Novemba 18/2021 hadi Desemba 14,2021.
Akizungumza
na waandishi wa habari wakati akitoa taarifa hiyo Kamanda wa Polisi
Mkoa wa Singida Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Stella Mutahibirwa
alisema kuwakamata mahalifu hao ni mafanikio makubwa kwa jeshi hilo.
Mutahibirwa
akizungumzia dawa za kulevya alisema katika kipindi hicho wamefanikiwa
kukamata madawa aina ya bhangi misokoto 667 na mbegu za bhangi kg. 1
ambapo walikamatwa watuhumiwa watatu, akiwemo mtuhumiwa wa kiume
anayetambulika kwa jina la Manjoli Manjoli (52) Mkazi wa Mtaa wa Utemini
Singida ambaye alikamatwa akiwa na misokoto 550 ya bhangi na kuwa
watuhumiwa hao ni wauzaji na watumiaji wa bhangi.
Alisema
katika msako huo pia yalikamatwa madawa ya kulevya aina ya mirungi
rumbesa 48 sawa na kg.26 pamoja na watuhumiwa wawili wanawake waliokuwa
wakiyasafirisha wakitokea mkoani Mwanza kuja Singida.
Aidha
Kamanda Mutahibirwa alisema katika msako huo walifanikiwa kuwakamata
watuhumiwa wanne wa wizi wa pikipiki ambao kesi zao zilishafikishwa
mahakamani ambapo vitu vingine vilivyopatikana ni video pc 2 na Radio
aina ya subwoofer 2.
Alisema
mafanikio hayo yametokana na taarifa za kiintelijensia zinazotolewa na
raia wema wanaopenda Mkoa wa Singida uendelee kuwa salama ambapo
alitumia nafasi hiyo kutoa wito kwa wananchi wote wa Mkoa wa Singida
kuendelea kutoa ushirikiano kwa kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu
zitakazosaidia kuwabaini watu wanaopanga kufanya uhalifu ili uhalifu huo
uzuiwe au watuhumiwa wakamatwe mapema kabla ya kuleta madhara.
"Wananchi
wanatakiwa kuachana kabisa na biashara haramu zikiwemo biashara za dawa
za kulevya aina mbalimbali badala yake wafanye kazi halali ambazo
ziotawapatia kipato" alisema Mutahibirwa.
Jeshi
la Polisi Mkoa wa Singida linawaomba wananchi wote waliopotelewa au
kuibiwa vitu kufika katika Kituo cha Polisi Singida wakiwa na risiti
halali za manunuzi ya vitu hivo ili kuweza kutambua mali zilizokamatwa.
Loading...
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi
==>>... << BOFYA HAPA Kui Install>>
Mgid
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )