Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Wednesday, December 8, 2021

Rais Samia aingia orodha wanawake 100 wenye ushawishi duniani


Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ametajwa kuwa miongoni mwa wanawake 100 wenye ushawishi mkubwa walioorodheshwa katika jarida la Forbes la wanawake wenye uwezo mkubwa duniani 2021, akishika nafasi ya 94.

Rais Samia ambaye aliingia kwenye wadhifa huo Machi, 2021 kutokana na kifo cha mtangaluzi wake hayati John Pombe Magufuli, ameingizwa kweneye orodha hiyo ambayo pia imemuweka aliyekuwa mke wa mtu Tajiri zaidi duniani Jeff Bezos, Mackenzie Scott kuwa katika nafasi ya kwanza.

Scott ambaye alitalakiana na bilionea Jeff Bezos na kuolewa na mwalimu ndiye mwanamke wa tatu Tajiri zaidi duniani.

Kwa mujibu wa jarida hilo maarufu, Rais Samia ameingia kwenye orodha hiyo akiwa amejipatia sifa kwa kufuata maagizo ya Uviko-19 na kuyaidhinisha nchini Tanzania.

Kwa mujibu wa muhariri wa Forbes orodha hiyo ya 18 ambayo hutolewa kila mwaka ya wanawake 100 wenye uwezo mkubwa duniani, inatoka katika mataifa 30 na inaangazia wanawake wanaofanya kazi katika idara za fedha teknolojia, siasa , uvumbuzi, burudani na zaidi, wote wakiwa na lengo moja.

Tangazo
ap
Loading...
taboola dsk
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )

End: