Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Saturday, December 11, 2021

Rais Samia ateta na Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika (AUC), Moussa Faki Mahamat

 Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, leo Jumamosi, tarehe 11 Desemba 2021, amefanya mazungumzo na Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika (AUC), Moussa Faki Mahamat, Ikulu jijini Dar es Salaam.

Taarifa juu ya mazungumzo hayo, imetolewa mchana wa leo kwa umma na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais-Ikulu, Jaffar Haniu.

Taarifa ya Haniu imesema kuwa, Rais Samia amemueleza Faki kwamba, Tanzania inajitahidi kukabiliana na athari za kiuchumi, zilizotokana na Ugonjwa wa Virusi vya Korona (UVIKO-19), ili kuhakikisha uchumi wake unaimarika.

“Rais Samia amesema ni wakati sasa kwa nchi za Afrika, kiutumia fursa zilizopo baada ya athari za UVIKO-19, kujiimarisha kiuchumi, kwa sababu nchi zina fursa nyingi kiuchumi,” imesema taarifa ya Haniu.

Katika mazungumzo hayo, mwenyekiti huyo wa Kamisheni ya AU, ameishauri Tanzania kuchangamkia fursa zinazopatikana katika Eneo Huru la Biashaea Afrika (AfCFTA)

Tangazo
ap
Loading...
taboola dsk
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )

End: