Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Wednesday, December 22, 2021

Viongozi CCM mbaroni kwa kumjeruhi Askari Polisi


Katibu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wilayani Babati Filbert Mdaki (52) na Katibu wa Jumuiya ya Vijana UVCCM wa Wilaya hiyo, George Sanka (46) wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kumpiga Askari Polisi mateke na fimbo.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Manyara, Benjamin Kuzaga, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo, ambapo amesema kuwa tukio hilo lilitokea Desemba 16 majira ya saa 11 jioni katika kijiji cha Kirudiki wilayani Babati.

Kamanda Kuzaga amesema watuhumiwa hao walimshambulia Koplo Baraka wa Kituo kidogo cha Polisi Kiru kwa mateke na fimbo baada ya kufika kwenye mkusanyiko wa wananchi wa Kijiji cha Kirudiki.

“Askari huyo baada ya kuona mkusanyiko alifika ili aulizie juu ya kibali cha mkusanyiko huo, ndipo viongozi hao wakamshambulia maeneo mbalimbali ya mwili,” amesema kamanda Kuzaga.

Amesema uchunguzi wa tukio hilo unaendelea na ukikamilika watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani.


Tangazo
ap
Loading...
taboola dsk
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )

End: