Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Saturday, December 11, 2021

Waziri Bashungwa awataka vijana kuacha chuki wanaposhindana kimaendeleo.


Na. Projestus Binamungu, WUSM
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Innocent Bashungwa amewataka wasanii kushindana bila chuki na uhasama katika kukuza muziki na biashara zao kwa manufaa yao na taifa kwa ujumla.

Waziri Bashungwa ametoa kauli hiyo wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa kampuni ya kubashiri ya WasafiBet iliyofanyika Mlimani City Desemba 10, 2021.

Akizungumza kabla ya uzinduzi huo Waziri Bashungwa amesema, kazi ya Serikali ni kuweka mazingira wezeshi kwa vijana wote na ndoto ya Serikali ni kuwaona vijana hao wakishindana kuwekeza kupitia karama zao bila chuki wala uhasama baina yao.

“Inapendeza tunapowaona mnashindana kimaendeleo bila chuki, na ningependa niwashauri vijana, tumieni karama zenu za ubunifu vizuri, msiweke chuki mnapopambana kujenga maisha yenu mimi ninaamini  mnaweza kushindana bila kutengeneza chuki au uhasama wowote.” Alisema Waziri Bashungwa

Alikadhalika Waziri Bashungwa ameeleza mchango wa michezo ya kubashiri katika maendeleo ya sekta ya michezo akisema Serikali inakusanya asilimia tano kutoka katika michezo hiyo na kueleza kuwa kuanzishwa kwa kampuni ya kubashiri ya WasafiBeti kutachangia moja kwa moja katika kuendeleza maendeleo ya michezo nchini.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa kampuni ya WasafiBeti Nasib Abdul maarufu kama Diamond ameitumia hafla hiyo kuishukuru Serikali kwa kujenga mazingira wezeshi kwa vijana wa kitanzania yanayotoa fursa ya kujishughulisha katika shughuli mbalimbali katika safari ya vijana wengi kutimiza ndoto zao.

“ Niseme tu ukweli, mafanikio ya Wasafi media ni kutokana na mazingira wezeshi ambayo sisi kama vijana tumejengewa na Serikali, unajua kwa √©limu yetu ndogo tuliyokuwa nayo Serikali imetubeba vizuri na kutuwekea mazingira ambayo yametufikisha hapa tulipo” alisema Diamond.

Kwa mujibu wa Diamondi ujio wa kampuni ya WasafiBeti unalenga kuboresha madhaifu yaliyopo katika michezo mingi ya kubashiri hapa nchini, pamoja na kutoa ajira kwa vijana na kuwapa kipato kupitia ubashiri watanzania na watu wote wanaopenda michezo.

Tangazo
ap
Loading...
taboola dsk
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )

End: