Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Thursday, January 13, 2022

Ashikiliwa Na Jeshi La Polisi Kwa Tuhuma Za Kumuua Baba Yake Mzazi Kwa Kisu


Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linamshikilia MUSSA EDWARD NDONDE @ SANGA MAPESA [31] Askari wa JWTZ MT.109772 Kikosi cha Ruvu JKT mkoani Pwani na Mkazi wa Mlandizi kwa tuhuma za kumuua baba yake mzazi aitwaye EDWARD NDONDE [75] Mwalimu Mstafuu, Mkazi wa Lumbila Jijini Mbeya kwa kumkatakata visu sehemu mbalimbali za mwili wake.  

Tukio hilo limetokea mnamo tarehe 12.01.2022 majira ya saa 09:00 asubuhi huko Mtaa wa Lumbila uliopo Kata ya Iwambi, Tarafa ya Iyunga, Jijini Mbeya ambapo mtuhumiwa aliuawa EDWARD NDONDE [75] ambaye ni baba yake mzazi kwa kumchoma kisu sehemu mbalimbali za mwili wake na kisha kumkata kiganja cha mkono.

Chanzo cha tukio ni tuhuma za ushirikina kwani inaelezwa kuwa mtuhumiwa anadai kuwa marehemu ambaye ni baba yake mzazi ni mchawi anamloga ili hasifanikiwe kwenye mambo yake. Awali  mtuhumiwa alifika nyumbani kwa marehemu majira ya 09:00 asubuhi pasipo kutoa taarifa  yoyote ya  kuja Mbeya na kuingia moja kwa moja sebuleni na kuanza kumshambulia kwa kisu na stuli na kupelekea kifo chake.

Mwili wa marehemu umehifadhiwa Hospitali ya Rufaa Kanda ya Mbeya kwa uchunguzi wa kitabibu. Mtuhumiwa anaendelea kupatiwa matibabu chini ya ulinzi Hospitali ya Rufaa Kanda ya Mbeya baada kushambuliwa na wananchi waliojichukulia sheria mkononi kutokana na tukio alilofanya.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linalaani tukio hili baya kutokea na litahakikisha mtuhumiwa anafikishwa kwenye mamlaka husika ya sheria kwa hatua zaidi. Aidha Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linatoa rai kwa wananchi kuachana na Imani potofu za kishirikina hasa kuamini waganga wapiga ramli chonganishi kwani ni hatari kwa ustawi wa jamii na maendeleo ya Taifa.

Imetolewa na:

[CHRISTINA A. MUSYANI – ACP]

KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

Tangazo
ap
Loading...
taboola dsk
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )

End: