Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Saturday, January 22, 2022

Balozi Mulamula Afanya Mkutano Kwa Njia Ya Simu Na Waziri Wa Mambo Ya Nje Wa Sweden


Na Mwandishi wetu, Dar

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula amefanya mkutano kwa njia ya simu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Sweden Mhe. Ann Linde katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam

Viongozi hao pamoja na mambo mengine, wamejadili masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Tanzania na Sweden ikiwemo vipaumbele vya pande zote mbili kuelekea Mkutano wa Wakuu wa Nchi baina ya nchi za Umoja wa Ulaya na Umoja wa Afrika (European Union – African Union Summit) uliopangwa kufanyika tarehe 17 – 18 Februari 2022.

Katika tukio jingine, Balozi Mulamula amekutana kwa mazungumzo na Balozi wa Somalia nchini Mhe. Zahra Ali Hassan katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam ambapo mazungumzo yao yamelenga kujadili masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Tanzania na Somalia

 

Tangazo
ap
Loading...
taboola dsk
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )

End: